Huduma ya SMS tayari inapatikana

Tuma SMS nyingi kwa biashara yako Tanzania.

Nisend inakusaidia kutuma bulk SMS, kupanga kampeni za matangazo na kuwapa wateja taarifa kupitia API ya SMS. Simamia mawasiliano, jina la mtumaji, salio na ripoti za ujumbe kwa kila biashara. Kwa WhatsApp Business, wasiliana na timu yetu.

Huduma zetu

Bulk SMS na maandalizi ya WhatsApp Business

Chagua njia inayofaa mawasiliano ya biashara yako.

Bulk SMS

Fikia mteja mmoja au maelfu.

Tuma SMS kupitia dashibodi au programu yako. Ingiza mawasiliano, unda makundi, hifadhi violezo na panga muda wa kutuma kampeni.

  • Uingizaji wa mawasiliano kutoka Excel
  • Sender ID iliyoidhinishwa
  • Historia ya ujumbe na ripoti za kufikishwa
Anza kutumia Nisend
WhatsApp Business

Tuzungumzie mahitaji ya biashara yako.

Timu yetu itakueleza kuhusu usajili wa namba ya biashara, mahitaji ya violezo na maandalizi ya kutuma ujumbe kwa wateja kupitia WhatsApp.

  • Maandalizi ya namba ya biashara
  • Mahitaji ya ujumbe na violezo
  • Bei na upatikanaji kupitia timu yetu
Wasiliana nasi kwa WhatsApp
Mawasiliano ya biashara

Matangazo, taarifa na vikumbusho kwa SMS

Huduma ya ujumbe mfupi kwa maduka, usafirishaji, huduma za miadi na biashara zinazohitaji kuwajulisha wateja.

SMS za matangazo na ofa

Wajulishe wateja kuhusu bidhaa, ofa na huduma mpya. Chagua kundi la mawasiliano, andika ujumbe na utume sasa au upange muda wa kutuma kampeni.

Taarifa za oda na usafirishaji

Unganisha API ya SMS na mfumo wako ili kuwajulisha wateja kuhusu oda, vifurushi na hatua za huduma. Fuatilia hali ya kila ujumbe kwenye historia ya SMS.

Vikumbusho kwa wateja

Tuma vikumbusho vya miadi, malipo na matukio kwa mawasiliano yako. Hifadhi violezo vya ujumbe unaotumia mara kwa mara ili kupunguza kazi ya kuandika upya.

Workspaces

Biashara tofauti. Akaunti moja.

Kila biashara, tawi au mteja ana eneo lake lenye mawasiliano, makundi, sender IDs, salio la SMS, API keys na historia ya malipo. Fuatilia matumizi ya kila biashara bila kuchanganya taarifa.

Kwa watengenezaji wa programu

API ya kutuma SMS na kufuatilia ujumbe

Unganisha Nisend na mfumo wa oda, usafirishaji au huduma kwa wateja. Tumia workspace API key kwenye seva yako, bila kuweka siri kwenye programu ya kivinjari.

SMS moja au nyingi

Tuma ujumbe kwa namba moja au kundi la hadi wapokeaji 5,000 tofauti kupitia REST API. Pata makadirio ya SMS kabla ya kutuma.

Salio na hali ya ujumbe

Soma salio la SMS na matokeo ya ujumbe au batch. Tumia idempotency key kuzuia majaribio yanayorudiwa kuunda ujumbe mwingine.

Webhooks na kumbukumbu

Pokea taarifa za Sent, Delivered na Failed kupitia webhooks zenye saini. Kagua maombi ya API na majaribio ya kutuma webhook kwenye workspace.

Bei na malipo

Nunua salio la SMS kulingana na mahitaji yako.

Weka kiasi cha fedha kwa TZS au idadi ya SMS unazohitaji. Utaona bei ya sasa, kiwango cha punguzo kinachotumika na salio utakalopata kabla ya kukamilisha malipo.

1. Chagua kiasi

Weka bajeti yako au idadi ya SMS kwenye ukurasa wa kununua salio. Huhitaji kuhesabu salio mwenyewe.

2. Lipa kwenye workspace

Tumia Mobile Money, Selcom Pesa au TANQR yenye msimbo wa QR na namba ya kulipia.

3. Fuatilia matumizi

Salio linaongezwa baada ya malipo kuthibitishwa. Historia ya manunuzi na ujumbe inapatikana kwenye workspace yako.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Unachohitaji kujua kuhusu Nisend

Ninawezaje kuanza kutuma SMS nyingi?

Fungua akaunti ya Nisend, tengeneza workspace ya biashara yako na nunua salio la SMS. Chagua jina la mtumaji linalopatikana, ongeza namba au kundi la mawasiliano, andika ujumbe na uhakiki makadirio kabla ya kutuma. Huduma ya bulk SMS tayari inapatikana.

Workspace ni nini?

Ni eneo maalumu la biashara moja ndani ya akaunti yako. Lina mawasiliano, makundi, majina ya watumaji, salio, ujumbe, funguo za API na historia ya manunuzi ya biashara hiyo. Unaweza kusimamia biashara zaidi ya moja kupitia akaunti moja.

Naweza kuingiza mawasiliano kutoka Excel?

Ndiyo. Pakua kiolezo cha Excel kwenye sehemu ya mawasiliano, jaza taarifa kisha pakia faili. Unaweza kupanga mawasiliano kwenye makundi au kuingiza namba mwenyewe unapounda ujumbe.

Bei ya SMS ni kiasi gani?

Bei ya sasa na viwango vya punguzo kulingana na kiasi cha ununuzi vinaonekana kwenye ukurasa wa kununua SMS. Weka kiasi cha fedha au idadi ya SMS unazotaka; mfumo utaonyesha jumla na salio utakalopata kabla ya kulipa.

Ninalipaje salio la SMS?

Unaweza kutumia Mobile Money, Selcom Pesa au TANQR. TANQR ina msimbo wa QR na namba ya kulipia. Salio huongezwa kwenye workspace yako baada ya malipo kuthibitishwa.

Naweza kutumia jina la biashara kama mtumaji?

Ndiyo. Omba sender ID kwenye workspace yako. Jina linaweza kuwa na hadi herufi, namba au nafasi 11, na lazima liwe na angalau herufi moja. Litatumika baada ya kuidhinishwa na mtoa huduma na kuwezeshwa na Nisend. Jina chaguomsingi likipatikana unaweza kulitumia wakati unasubiri ombi lako.

Kwa nini ujumbe mmoja unaweza kutumia SMS zaidi ya moja?

Ujumbe mrefu na baadhi ya alama, kama emoji, zinaweza kuhitaji vipande kadhaa vya SMS. Nafasi na mistari mipya pia huhesabiwa. Sehemu ya kuandika ujumbe inaonyesha idadi ya herufi na makadirio ya SMS; kutuma kwa watu wengi kunategemea pia idadi ya wapokeaji.

Hali za Queued, Sent, Delivered na Failed zina maana gani?

Queued: ujumbe unasubiri kuwasilishwa kwa mtoa huduma. Sent: mtoa huduma ameupokea, lakini matokeo ya mwisho bado yanasubiriwa. Delivered: taarifa ya kufikishwa imeripotiwa. Failed: kushindwa kufikishwa kumeripotiwa. Taarifa ya mwisho inaweza kuchelewa hata kama SMS tayari imefika kwenye simu.

Ninawezaje kuunganisha API ya SMS?

Tengeneza API key ya workspace yako na uitumie kwenye seva ya programu yako. API inawezesha kutuma SMS moja au nyingi, kupata makadirio ya salio, kusoma salio na kufuatilia hali za ujumbe. Weka webhook ili kupokea mabadiliko ya hali; historia ya maombi na majaribio ya webhook inapatikana kwenye workspace.

Huduma ya WhatsApp Business inapatikanaje?

Wasiliana nasi kupitia 0744 958 059 kwa maandalizi ya WhatsApp Business. Tutajadili namba ya biashara, mahitaji ya kuanza, violezo, upatikanaji na bei. WhatsApp haiwezeshwi moja kwa moja unapofungua workspace ya SMS, na salio la SMS halitumiki kwa WhatsApp.

Wasiliana nasi

Unahitaji WhatsApp Business?

Tuambie kuhusu biashara yako na ujumbe unaotaka kutuma. Tutakusaidia kuelewa hatua za kuanza, mahitaji na bei.

Wasiliana kwa WhatsApp +255 744 958 059